Leo July 30,2018 tunayo story kutokea Mahakama ya Wilaya ya Ilala, ambapo Madiwani 2 wa CHADEMA na mmoja wa chama cha CUF, wamefikishwa mahakamani hapo wakikabiliwa na mashtaka 2 ikiwemo kushawishi rushwa ya Sh.Mil 25 na kupokea rushwa ya Shilingi Milioni 3 kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya M/S M+M Architects Co. Ltd
Madiwani hao ni Diwani wa Kata ya Segerea, Edwin Mwakatobe (33) na Diwani wa kata ya Mchikichini Joseph Ngowa (45) wote CHADEMA na Diwani wa Kata ya Mnyamani kupitia CUF, Shukuru Dege (42)
Katika kesi hiyo ya jinai namba 420 ya 2018 washtakiwa wamesomewa mashtaka yao na Wakili wa TAKUKURU, Devotha Mihayo mbele ya Hakimu Mkazi, Flora Mujaya.
Katika kesi hiyo kosa la kwanza linamkabili Mwakatobe ambapo anadaiwa July 2018 akiwa katika Wilaya Ilala, kama Diwani wa kata ya Segerea na mjumbe wa kamati ya Fedha na Utawala katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala alishawishi rushwa ya Sh.Mil 25 toka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya M/S M+M Architects Co. Ltd, Burhan Mvungi kama kichocheo cha kupendelewa katika tenda na LG/015/2017/2018/HQ/CS/07 Lot 03 ambayo ilikuwa chini ya muajiri wao.
Shtaka la pili inadaiwa kuwa madiwani hao, Mwakatobe, Ngowa na Dege July 24, 2018 katika Baa ya Kwetu Pazuri iliyopo Tabata Wilaya ya Ilala, wote wakiwa wajumbe wa kamati ya fedha na utawala ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala walipokea rushwa ya Sh.Mil 3 toka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya M/S M+M Architects Co. Ltd, Burhan Mvungi kama kichocheo cha kupendelewa katika tenda na LG/015/2017/2018/HQ/CS/07 Lot 03 ambayo ilikuwa chini ya muajiri wao.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo washtakiwa hao waliyakana ambapo waliomba dhamana na upande wa mashtaka haukuwa na pingamizi la dhamana.
Hakimu Mujaya alimtaka kila mshtakiwa kuwa na wadhamini 2 ambao wana barua kutoka katika sekta ambayo inatambulika na kila mdhamini asaini bondi ya Sh.Mil 1.
Baada ya kutolewa kwa masharti hayo mshtakiwa Mwakatobe na Ngowa walikamilisha masharti ya dhamana na kuachiwa, huku mshtakiwa Dege akirudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti hayo.
Kesi imeahirishwa ahadi August 13 , 2018 kwa ajili ya kutajwa.
LIVE MAGAZETI: Siri nje Jokate kuteuliwa, Mnyukano CCM asilia, Wahamiaji