PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Top Stories

RAIS MAGUFULI AMLILIA MZEE MAJUTO “SITOSAHAU UCHESHI WAKE”

on

Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kufuatia kifo cha msanii mkongwe hapa nchini Mzee Amri Athuman maarufu kwa jina la King Majuto.

Rais Magufuli amesema King Majuto atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa na wa muda mrefu alioutoa kupitia sanaa ya uigizaji na uchekeshaji, ambapo alishiriki kuelimisha jamii, kuendeleza na kukuza sanaa na kuunga mkono juhudi za chama na Serikali katika kuhimiza maendeleo.

“King Majuto alikuwa kielelezo cha safari ndefu ya sanaa kwa nchi yetu, kwa muda wote amedhihirisha kipaji, ujuzi na uwezo wa hali ya juu katika uigizaji na uchekeshaji na hivyo kuwa kipenzi cha Watanzania na wasanii wenzake, hatutasahau ucheshi wake, upendo na uzalendo kwa nchi yake wakati wote wa uhai wake” Rais Magufuli.

BREAKING: Kinachoendelea Muhimbili kifo cha Mzee Majuto

 

Soma na hizi

Tupia Comments