PremierBet Tanzania Usain Bonus Ad

AyoTV

Niyonzima Man Of The Match “Nikipewa nafasi nitaitendea haki”

on

Simba SC wamefanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Mlandege goli ambalo limefungwa na Haruna Niyonzima dakika ya 21 ya mchezo kwa penati, hivyo Simba imemaliza game zake za Kundi B ikiwa imepata ushindi katika michezo yao yote mitatu na kuvuna jumla ya point 9.

Baada ya game hiyo Haruna Niyonzima aliyekuwa nahodha wa Simba SC katika game ya leo dhidi ya Mlandege FC, alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mechi (Man Of The Match”, aliongea na waandishi wa habari na kuzungumza mambo mbalimbali katika soka lake.

“Hakuna mechi ndogo sisi malengo yetu yalikuwa kushinda mechi tatu nashukuru Mungu tumetimiza japokuwa Mapinduzi hayajaisha, kitu ambacho kocha alifanya vizuri ni kuleta wachezaji wote ambapo tumetumia michuano hii kama sehemu ya maandalizi yetu, nikipewa nafasi ya kuanza nitaitendea haki lakini nisipopewa basi nitawaombea lakini mwalimu ndio mwenye uamuzi”>>>Haruna Niyonzima

Mpenja katangaza goli kabla ya kona kupigwa, ataomba kutotangaza game za timu yake

Soma na hizi

Tupia Comments