Tangaza Hapa Ad

AyoTV

EXCLUSIVE: Kijana aliyemshtua Mama Kanumba, maneno 30 ya Dully Sykes kuhusu Alikiba

on

Ni time ya AyoTV Entertainment ambapo Asteria Mvungi anakukutanisha na stori za mastaa wa bongo na kauli zao, Dully Sykes kuhusu kushirikiana na Alikiba, Mama Kanumba kamuweka wazi mrithi wa Marehemu Steven Kanumba.

Mama Kanumba kwa mara ya kwanza amemuonyesha kijana ambaye amefanana sana kimuonekano na mwigizaji marehemu Steven Kanumba aliyefariki April 2012 ambapo amesema kwa miaka yote hiyo toka kifo cha Kanumba kulikua na vijana wanakuja na kusema wamefanana na Kanumba lakini hakuwakubali, huyu wa leo ndio wa kwanza.

Namnukuu >>> ‘Ni kweli huyu kijana kimuonekano, kinidhamu anafanana na kuendana na marehemu Kanumba japokua watu hawawezi kufanana vitu vyote, huyu kijana ndio mimi natangaza kwa mara ya kwanza kuwa ndio mrithi wa Kanumba’

Kwenye video hapa chini utamuona huyo kijana mwenyewe.

Dully Sykes amezungumzia ufanyaji kazi wake na mwimbaji Alikiba na kusema kwamba Ali ndio alikua awepo kwenye nafasi ya Ommy Dimpoz kwenye single ya ‘utamu’ ambayo pia Diamond Platnumz alitokea lakini ikashindikana.

Nilimuita Dimpoz baadae baada ya Alikiba kuwa na mambo mengi lakini hana matatizo na mimi, ni mtu ambae napatana nae sana tuko pamoja na hakuna shida na yeye‘ – Dully

Tazama hii video hapa chini kutazama full video…

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement