Michezo

Alikiba kafika mazoezi, Kocha kafunguka “kamaliza kutafuna karanga sasa apige mluzi” (+video)

on

Mchezaji na Mfadhili  wa Timu  ya  Coastal Union, Wagosi wa kaya Ally Salehe Kiba (AliKiba) amesema kwasasa yupo tayari kuitumikia Klabu hiyo mara baada ya kumaliza majukumu  yake ya kimuziki ndani na nje ya nchi hivyo kwasasa anatekeleza programu za mwalimu ambaye  ndiye anajua nini anapaswa kufanya ili kujenga team work baada ya kukosekana kwa muda mrefu.

Naye Kocha wa Timu hiyo ya Wagosi wa kaya Juma Mgunda amesema kwasasa Kiba  anaprogramu maalumu ambayo kama ataifanya vizuri anauwezo wa kuingia katika kikosi cha kwanza.

MAMA KAFUNGUKA “DOGO JANJA NI KILA KITU KWANGU, NAUMIA AKITUKANWA”, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA
https://youtu.be/mYP8OGE75OE

Soma na hizi

Tupia Comments