Top Stories

“Mkurugenzi ukirudi hakikisha unarudi na kichwa cha mtu” Mwijage

on

Leo July 12, 2018 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage na Waziri wa Kilimo Charles Tizeba wapo mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi, ambapo wametembelea maeneo ya mpaka wa Tanzania na Uganda (Mtukula) na kukuta Taasisi za serikali zikitajwa kuonea wananchi wakati wa kutoa huduma.

Wakiongea na wafanyabiashara wa maeneo hayo, Waziri Mwijage amemuagiza Kaimu Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko Taifa Wilson Malosha kurudi katika maeneo hayo na kuchunguza mambo yanayofanywa na watendaji walioko chini yao ili wachukuliwe maamuzi magumu na kuongeza kuwa lazima akirudi arudi na kichwa cha mtu, ukishindwa patakuwa hapakutoshi hapo.

WhatsApp ilivyookoa maisha ya Mama Mjamzito Lindi

Soma na hizi

Tupia Comments