Tangaza Hapa Ad

AyoTV

VIDEO: ‘Nilikwepa mawe manne kabla ya kuchomwa mkuki mdomoni’-Augustine Mtitu

on

Moja ya tukio lililomake headline wiki hii ni kuhusu mkulima, Augustino Mtitu aliyechomwa mkuki mdomoni na ukatokea shingoni kwa kile kilichoelezwa ni mgogoro wa wakulima na wafugaji huko kijiji cha Dodoma Isanga kata ya Manzese wilaya ya Kilosa Mororgoro.

AyoTV na millardayo.com ilifika hospitali ya mkoa wa Morogoro ambako mkulima huyo anaendelea na matibabu na kuzungumza naye ambapo alisimulia hali ilivyokuwa.

‘Kuna wafugaji waliingiza ng’ombe kwenye shamba la jirani, kijana mmoja akatoka wakamchapa fimbo, nilipoenda kusaidia wakaanza kunishambulia kwa mawe, nikakwepa mawe manne na nilipotaka kugeuka nikimbie nikashtukia mkuki umenichoma mdomoni’;-Augustino Mtitu

VIDEO; Taarifa ya jeshi la polisi DSM kuhusu matukio yote ya mwaka 2016 , Bonyeza play hapa chini kutazama

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement