Tangaza Hapa Ad

Mix

Mke wa Donald Trump hatishi Ikulu ya White House mpaka June 2017

on

Mke wa Rais mteule wa Marekani Donald Trump, Melania Trump hataishi Ikulu kwasababu ya mtoto wao mwenye umri wa miaka 10, Barron Trump ambaye yuko shule kwenye mji wa New York na itakuwa ngumu kumuhamisha mpaka atakapomaliza masomo yake.

TMZ walinukuu maneno ya Trump alieeleza juu ya taarifa hii

“Melania hataki kusumbua maisha ya mtoto wakati bado hajamaliza shule kwahiyo bado wataishi kwenye jumba la Trump Tower New York mpaka June 2017 ndipo watahamia Ikulu, kwasasa hawezi kumuweka mtoto wake mbali na marafiki zake, michezo na shule yake’ – Donald Trump

Trump alisema Melania atakuwa akienda Ikulu akimuhitaji na kurudi nyumbani New York lakini mtoto hatohangaishwa mpaka amalize shule mwanzoni mwa June 2017 na hakuna kitakachobadilishwa kwenye kauli hii kwani wameshaamua hivyo kama familia.

103173967

Melania akiwa na mtoto wake Barron

VIDEOTazama hapa chini show ya Diamond iliyovunja rekodi Marekani

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement