Top Stories

Mume wa Amber Rutty aanguka Mahakamani | Hakimu aahirisha kesi

on

January 10, 2018 Mume wa msanii Rutyfiya Abubakary maarufu kama ‘Amber Rutty’ ambaye ni Said Mtopali amedondoka ghafla katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu muda mfupi baada ya kesi yao kuahirishwa.

Amber Rutty na Mumewe walifikishwa Mahakamani hapo November 2, 2018 wakikabiliwa na kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

Mbali na wawili hao, Mshtakiwa mwingine ni James Charles maarufu kama ‘James Delicious’.

Kesi ya Washtakiwa hao imeahirishwa mbele ya Hakimu Mkazi Janeth Mbando hadi February 11,2019 baada ya Wakili Neema Mbwana kusema upelelezi haujakamilika.

Baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, Washtakiwa hao walianza kuondoka katika viwanja vya Mahakama hiyo ambapo Mtopali wakati anashuka kwenye ngazi ndipo alipoanza kujisikia vibaya na ghafla kudondoka.

Kutokana na hatua hiyo watu mbalimbali wakiwemo ndugu zake walianza kumpepepea ili kumpatia msaada wa kwanza lakini baadaye walimtoa katika viwanja vya Mahakama hiyo ili kumpeleka hospitali.

Katika kesi hiyo kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile linamkabili Amber Rutty, ambapo anadaiwa amelitenda kati ama baada ya October 25, 2018 ambapo alimruhusu Said Bakary kumuingilia kinyume na maumbile, kosa ambalo amelikana.

Pia kosa jingine la kufanya mapenzi kinyume na maumbile, linamkabili mshtakiwa wa pili Said Bakary ambapo anadaiwa kati ama baada ya October 25,2018 jijini DSM alifanya mapenzi na Amber Rutty kinyume na maumbile ambapo alisema si kweli.

Kosa la tatu la kuchapisha video ama picha za ngono, ambapo linamkabili James Charles ama James Delicious akidaiwa kati ya October 25,2018 alisambaza video za ngono kupitia magroup ya Whatsapp.

Kosa jingine la nne ni kusababisha kusambaa picha za ngono linamkabili Amber Ruth na Said Aboubakary ambapo wanadaiwa kati October 25,2018 walisababisha kusambaza picha za ngono kupitia makundi ya Whatsapp. Kosa ambalo wamesema si kweli.

RC MWANRI AMVAA MHINDI KISA WAFANYAKAZI “WHERE IS MIKATABA NOW, BISHA UONE”

Soma na hizi

Tupia Comments