PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Top Stories

Polisi Mexico kutumia Manati badala ya bunduki

on

Leo July 11,2018 nakusogezea stori hii kutoka huko nchini Mexico ambapo Gavana wa mji wa Veracruz Miguel Angel amewataka Polisi katika mji wake kuanza kutumia Manati kukabiliana na wahalifu badala ya kutumia bunduki.

Imeelezwa kuwa Gavana Miguel amechukua uamuzi huo baada ya Polisi 30 kati ya 130 kufaulu jaribio la kutumia bunduki na kudhihirsha kuwa Maafisa wengi wa Polisi hawajui kutumia bunduki vizuri kitu ambacho ni hatari kwa usalama wa Raia.

Imedaiwa kuwa miji mingine mathalani Ciudad Mendoza, Pueblo Viejo na Ixtaczoquitlan ya chini humo nayo imewakataza Polisi wake kutumia bunduki badala yake imewagawia Manati ili kukabiliana na wahalifu.

Aidha maamuzi hayo ya Gavana Miguel yamekosolewa sana na Meya wa mji huo kwa madai kwamba Polisi kutumia Manati kuwalinda Watu na mali zao ni kichekesho kwani hawatoweza kukabiliana na wahalifu wanaotumia silaha kali.

BREAKING: Ambulance imekamatwa na KILO 800 za Dawa za Kulevya

Soma na hizi

Tupia Comments