Michezo

Shabiki akubali kuishabikia Manchester UTD ili aongezewe Damu

on

Leo June 4, 2018 nakusogezea stori toka nchini Uingereza ambapo shabiki mmoja wa Chelsea aliyekuwa akihitaji kuongezewa damu amejikuta akibadili timu ya kushabikia baada ya kupewa sharti la kuanza kuishabikia Manchester United ili apewe damu hiyo na kaka yake.

Martin Warbuton ambaye ni shabiki ndakindaki wa mashetani wekundu alimpa sharti ndugu yake Paul ambaye ni mshabiki wa Chelsea la kuhama timu ya kushabikia huku wakitia saini kabisa ili mmojawapo asije akamgeuka mwenzake.

Paul aligundulika kuwa ana kansa ya damu hivyo alihitaji damu hiyo ya ndugu yake kusaidia kutatua tatizo lake la afya.

Aidha ndugu hao kwa miaka mingi wamekuwa wakibishana kuhusiana na timu wanazoshabikia huku kila mmoja akiona timu yake ni nzuri zaidi ya mwenzake na ndio maana Martin aliamua kumfanyia ndugu yake huyo ili kumaliza ubishi wa nani anashabikia timu bora.

Mengi tusiyoyajua ya Maria na Consolata anazungumza Mwalimu wao ‘Kuchunguliana Mitihani Je?’

Soma na hizi

Tupia Comments