PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Michezo

“Waingereza hawakutuheshimu sisi”-Luka Modric

on

Moja kati stori zilizochukua headlines sana kwa sasa katika soka ni game ya nusu fainali ya pili kati ya England dhidi ya Croatia, kwani baada ya England kutolewa katika michuano hiyo kwa kipigo cha magoli 2-1 dhidi ya Croatia, kimewashangaza wengi kwani hawakutarajia.

Mashabiki wengi wa England waliyokuwa Urusi na hata England walikuwa wameanza kushangilia kwa kauli yao ya “Its Coming Home” wakiashiria kuwa Kombe linakuja nyumbani, huku mashabiki wengine wakichora tattoo za kuonesha kuwa England Bingwa tayari.

Bahati mbaya mambo yamekuwa tofauti na England wametolewa kwa kufungwa goli 2-1, hivyo ndio mwisho wa ndoto yao baada ya game hiyo nahodha wa Croatia Luka Modric aliongea na waandishi wa habari na kuwaeleza kuwa England waliwachukulia poa.

“Waliidharau Croatia usiku wa leo na ndio lilikuwa kosa lao kubwa maneno yote hayo kutoka kwao tuliyasoma na kusikia na tukasema tutatona nani atachoka leo, hatukuchoka na tulimiliki mpira kiakili na kimwili kama nilivyosema awali walipaswa kuwa wapole na kuheshimu timu pinzani”>>> Luka Modric


Haji Manara kaeleza sababu za kuwasajili Wawa, Dida na Kagere

Soma na hizi

Tupia Comments