Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Alvaro Morata kashindwa kuheshimu maamuzi ya Antonio Conte

on

Moja kati ya habari zilizochukua headlines kuelekea mchezo wa Chelsea dhidi ya FC Barcelona katika uwanja wa Stamford Bridge ni pamoja na tabia ya Alvaro Morata aliyoionesha kabla ya game ya FC Barcelona na Chelsea kuanza.

Kwa mujibu wa mchezaji wa zamani wa Chelsea na mchambuzi wa BT Sport Glenn Hoddle aliyekuwa akiripoti game hiyo kutokea uwanjani, ameripoti kuwa Morata hakuonesha tabia nzuri wakati timu zikifanya warm up kutokana na kutokuwa katika kikosi cha kwanza, baada ya kocha wake Antonio Conte kumchezesha Hazard nafasi yake.

Kocha wa Chelsea Antonio Conte aliamua kumchezesha Eden Hazard nafasi ya mshambuliaji badala ya kiungo na sio kumtumia mshambuliaji asilia katika eneo hilo ambaye ni Alvaro Morata, hivyo Morata alionesha tabia ya kutofurahishwa na maamuzi ya kocha ila baadae aliingia dakika ya 83 akitokea benchi.

Mastaa wa soka Bongo Niyonzima, Kaseja, Okwi, Manula na Himid wakiwa na wake zao

Soma na hizi

Tupia Comments