Tangaza Hapa Ad

HekaHeka

HEKAHEKA: Undani wa ishu ya Mke kuwamwagia mafuta ya moto Mume na Mtoto

on

Leo January 30 2017 kupitia Leo tena ya Clouds FM Geah Habib ametuletea moja ya hekaheka ambayo ilikuwa gumzo wiki iliyopita inayomuhusu Mwanamke aliyewamwagia mafuta ya moto mume na mtoto kisa kapewa talaka.

Geah Habib amemuhoji Mume mwenyewe aliesema ‘ishu ni watoto ambao amewakuta hasa wa kiume ambapo kabla alikuwa anaigiza kumpenda kwa sababu wakati namtongoza nilimpeleka nikamuonyesha mwanangu huyu hapa ila sina mawasiliano mazuri na mama yake’

‘Mabadiliko yalikuja nilipojenga…. nilitaka nimfanyie surprise akute imeisha, siku nimekwenda naye akaropoka sitaki kumuona hapa Rama’

‘Nilikuwa nimempa talaka siku mbili hakuondoka nyumbani, mlango wa chumbani niliufunga nikapiga na misumari, mimi nilikuwa nimelala fofofo na mtoto akapitia juu, nilistukia moto nikapiga kelele nikajiburuza mpaka kwa majirani nikawaambia wakamwangalie mtoto, mtoto nae kaungua’

Bonyeza play hapa chini kusikiliza Full stori

Ulikosa? Hekaheka ya aliyechoma visu ovyo watu wa Mabibo Dar es salaam, Bonyeza play hapa chini kusikiliza  

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement