Tangaza Hapa Ad

Michezo

Matokeo ya derby ya mchezo wa ufunguzi Mapinduzi Cup 2017 Zanzibar

on

Usiku wa December 30 2016 visiwani Zanzibar mchezo wa ufunguzi wa michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa mwaka 2017 ndio ulichezwa visiwani hapo kwa kuzikutanisha timu za Jang’ombe Boys dhidi ya Taifa Jang’ombe katika uwanja wa Amaan.

Huu ni mchezo ambao ulikuwa unazikutanisha timu zilizokuwa zinaunda timu moja hapo awali kabla ya kuamua kutengana, kitu ambacho kimeufanya mchezo huu kuwa na mvuto wa kipekee.

img-20161231-wa0006

Mchezo huu kwa hapa Unguja unahesabika kama ni mchezo wa derby kama ilivyo kwa Dar es Salaam timu za Simba na Yanga, haukuwa mchezo rahisi kufungana lakini dakika ya 83 Hassan Seif ndio aliamua matokeo ya mchezo kwa kuifungia timu yake ya Taifa Jang’ombe goli pekee lililoufanya mchezo kumalizika kwa Taifa Jang’ombe kuibuka na ushindi wa goli 1-0.

img-20161231-wa0008

Taifa Jang’ombe sasa watarudi uwanjani Jumapili ya January 1 2016 saa 20:30 usiku kucheza dhidi ya Simba katika uwanja wa Amaan ila kwa siku ya Jumamosi ya December 31 hakutakuwa na mchezo wowote wa Kombe la Mapinduzi.

ALL GOALS: JKT Ruvu vs Yanga December 17 2016, Full Time 0-3

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement