Tangaza Hapa Ad

Michezo

Good news mtanzania mwingine anayekwenda kucheza soka Ulaya (+Audio)

on

Kama unapenda soka la bongo muda wowote kutokea sasa tegemea kusikia good news kutoka kwa mtanzania Hamisi Mroki anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya Kabin United ya daraja la pili Thailand.

Baada ya kuitumikia timu hiyo kwa misimu mitatu Hamisi amefanikiwa kumaliza mkataba wake na kupata timu mpya ya daraja la kwanza nchini Ukraine, good news ni kuwa Hamisi anaenda kujiunga na timu hiyo moja kwa moja na wala sio kufanya majaribio, millardayo.com imempata katik exclusive kutokea Thailand.

“Kwa sasa nimemaliza mkataba na timu yangu ya zamani ya Kabin United ya daraja la pili hapa Thailand, nimeitumikia kwa misimu mitatu na kwa sasa nimemaliza nayo mkataba na naenda kucheza Ukraine katika timu ya daraja la kwanza nipo katika mchakato wa kukamilisha baadhi ya taratibu” >>> Mroki

Kama dili la Hamisi kujiunga na timu ya daraja la kwanza Ukraine litafanikiwa itakuwa ni good news kwake na kwa soka la bongo maaana atakuwa amepiga hatua, kutoka kucheza soka katika nchi iliyo nafasi ya 129 katika viwango vya FIFA na kwenda kucheza nchi iliyopo nafasi ya 37 katika viwango vya FIFA duniani.

VIDEO: Msimamo wa Simba uliyotolewa leo kuhusu point 3 vs Kagera Sugar

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement