Tangaza Hapa Ad

Michezo

Yanga sasa wanaisubiri Azam FC, wamemalizana na Zimamoto kwa ushindi

on

Michuano ya Kombe la Mapinduzi imeendelea tena leo January 4 2017 kwa Yanga kucheza mchezo wake wa pili wa Kombe la Mapinduzi Cup dhidi ya Zimamoto katika uwanja wa Amaan Zanzibar.

Yanga ambao mchezo uliyopita walipata ushindi wa goli 6-0, leo January 4 2017 wamepata ushindi mwingine kwa kuifunga Zimamoto goli 2-0, magoli yakifungwa na Simon Msuva dakika ya 11 na 21 huku akikosa penati kipindi cha pili, Msuva pia ametangazwa na mchezaji bora wa mchezo.

Yanga anaendelea kuongoza Kundi B kwa kufikisha jumla ya point 6 na magoli nane huku akiwa hajaruhusu kufungwa goli hata moja katika michuano hii, lakini wamesalia na mchezo mmoja dhidi ya Azam FC watakaocheza nao January 7 saa 20:15 uwanja wa Amaan.

ALL GOALS: JKT Ruvu vs Yanga December 17 2016, Full Time 0-3

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement