Tangaza Hapa Ad

AyoTV

VIDEO: ‘Polisi mkikuta mtu kwenye msitu piga, haki za binadamu waje kwangu’ -RC Makonda

on

August 25 2016 baadhi ya viongozi wa Serikali akiwemo Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda wameungana na watanzania wengine kuaga miili ya Askari Polisi waliofariki kwa kupigwa risasi katika shambulio lililotokea Mbande, Dar es salaaam usiku wa August 23 2016.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ni miongoni mwa viongozi waliosimama kuongea ambapo amesema…>>>’Hatujapata taarifa kwamba majambazi waliohusika wanatoka nchi nyingine maanayake ni ndugu zetu wanaoishi kwenye majumba yetu‘ –RC Makonda

Askari mmoja analinda watu zaidi ya 500 kwamaana hiyo kupoteza askari wanne maana yake wananchi wasiopungua 6000 wanakaa bila ulinzi, natoa wito kwa wanaojiita haki za binadamu‘ –RC Makonda

Askari ukikutana na mtu yoyote kwenye msitu wewe piga alafu hao haki za binadamu waje kwangu, hatuwezi kuishi kwenye mkoa kama huu wakati Askari wetu tunawaondoa na natoa wito kama kuna haki za binadamu basi nataka haki za askari wangu kwanza‘ –RC Makonda

Unaweza kuendelea kumsikiliza RC Makonda kwenye hii video hapa chini…

 ALIYEJERUHIWA KWA RISASI KWENYE MAUAJI YA POLISI AMEYAONGEA HAYA

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement