Premier Bet
TMDA Ad

Top Stories

RC Makonda afika eneo lenye mafuriko “tunapajenga upya Jangwani” (+video)

on

Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda leo amefanya ziara ya ukaguzi wa athari za mafuriko ambapo amesema serikali imeanza kukarabati miundombinu iliyoathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha ikiwemo madaraja, barabara, mito na mifereji.

RC Makonda amesema miongoni mwa maeneo yanayoboreshwa na pesa ipo tayari ni mto Msimbazi wenye urefu wa KM 19 na eneo la Jangwani ambalo maboresho yake yatagharimu zaidi ya Bilioni 200 ikiwa ni mkopo kutoka Bank ya Dunia.

Aidha RC Makonda amesema hadi sasa jumla ya watu wawili wamefariki kutokana na mvua ambapo amewapa pole wananchi waliokumbwa na athari za mafuriko ikiwemo wale ambao mali zao zimeharibiwa na wengine kulazimika kuyaama makazi yao.

Pamoja na hayo RC Makonda amewataka wananchi wanaoishi maeneo hatarishi kuhama huku akiwataka wakazi wa jiji hilo kufanya usafi katika mazingira yao ili kuepuka magonjwa ya mlipuko.

Katika hatua nyingie RC Makonda amewataka wananchi kuchukuwa tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Dengue kwa kuhakikisha wanatokomeza mazalia ya mbu na kuhakikisha wanawahi vituo vya afya pindi wanapoona dalili za homa.

Kamanda Mwanza na taarifa za Mtu kujirusha ghorofani bila kutokwa damu wala kuvunjika

Soma na hizi

Tupia Comments