Premier Bet

Top Stories

Mambo kumi usiyoyajua kumhusu Idi Amin utabaki mdomo wazi (+video)

on

Leo June 12, 2019 nakusogezea Mambo 10 kumhusu aliewahi kuwa Rais wa Uganda Idi Amin hapa nakuwekea machache tu ila full story ipo kwenye video hapa chini.

1.Aliwahi kuwa bingwa wa ndondi wa uzito wa juu nchini Uganda mwaka 1960-1961

2.Alijichagua kuwa Rais wa Uganda kwa mapinduzi ya kijeshi, na waganda wengi walimchukulia kuwa ni shujaa kwa kumuondoa rais walieona “anasuasua” Milton Obote mwaka 1971.

3.Aliua watu zaidi ya laki tatu (300,000) kwa kipindi cha miaka 8 aliyokuwepo madarakani kabla ya Kung’olewa na Majeshi ya kitanzania mwaka 1979 baada ya kutaka kuteka sehemu ya Tanzania.

4.Aliwatimua raia wote wenye asili ya Kihindi nchini kwake na kutaifisha mali zao zote.

5.Alijipa vyeo kibao na kujiita Field Marshall Al Hadj Doctor Idi Amin Dada!

6.Inasemekana alimtumia Malkia wa Uingereza Elizibeth II barua za kimapenzi akimuomba amuoe ili aweze kujiita mfalme kwani alikuwa ameshajipa vyeo vyote kasoro “King” Yaani Mfalme.

7.Ana watoto zaidi ya 40 huku akiwa ameoa wake 6, mmoja wa wake zake alikutwa ameuawa kinyama baada ya kupata ujauzito na mtu mwingine.

8.Vyombo kadhaa vya Habari vimekuwa vikimuhusisha na ulaji wa nyama za watu hasa maadui zake aliowaua.

9.Licha ya ukatili dhidi ya binadamu, Idi Amin hajawahi kufikishwa Mahakamani mpaka anakufa mwaka 2003 na kuzikwa nchini Saudi Arabia alikokuwa akiishi uhamishoni.

10. Hajawahi kuandika popote historia ya maisha yake wala kuruhusu mtu yeyote Yule kuandika kuhusu maisha yake!.

WATU MAARUFU WALIOZALIWA TANZANIA LAKINI SIO WATANZANIA

Soma na hizi

Tupia Comments