Tangaza Hapa Ad

Mix

Wanafunzi wadaiwa kumng’oa meno Mwalimu, kisa…….

on

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.

Kati ya stori kubwa ambazo zimeandikwa kwenye magazeti ya leo ni hii ya kwenye gazeti la Tanzania Daima yenye kichwa cha habari,Wanafunzi wamng’oa meno matano mwalimu wao’

Wanafunzi kidato cha sita shule ya sekondari Usevya Halmashauri ya Mpwimbwe wilayani Mlele Katavi wamewacharaza viboko walimu wawili na kung’oa meno matano makamu mkuu wa shule hiyo, Makonda Ng’oka Membele.

Mwalimu mwingine aliyekumbana na kichapo hicho, Gabriel Kambona huku ikielezwa sababu za kuwapiga walimu hao ni kutokubali kufundishwa na mwalimu Membele kwa maaia kwamba ana tabia ya kuwadhalilisha wanafunzi wa kiume.

May mwaka huu mwalimu huyo alifikishwa katika mahakama ya wilaya ya Mpana kwa tuhuma za kumlawiti mwanafunzi wake akidaiwa kutenda kosa hilo kati ya November mwaka jana na April mwka huu.

Inadaiwa kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa mwalimu Ng’oka kulitokana na wanafunzi hao kumkataa na kutishia kuandamana kupinga vitendo vyake vya kuwalawiti wanafunzi.

Wanafunzi hao walidai kuwa mwalimu huyo amekuwa akiwalawiti baadhi yao ikiwa ni adhabu mbadala wanapobainika kufanya makosa shuleni hapo.

Hata hivyo baada ya kutopatikana kwa ushahidi wa kumtia hatiani mwalimu huyo, July 27 mwaka huu mahakama hiyo ilimuachia huru na August mosi alirudi kwenye kituo chake cha kazi ambapo iliwakera wanafunzi hao na kutaka mwalimu huyo aondoke.

Source: Tanzania Daima

ULIKOSA UFAFANUZI KUHUSU VIPIMO VYA MATETEMEKO YA ARDHI VILIVYOIBIWA? BONYEZA PLAY HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement