AyoTV

Maneno ya Mwigulu Nchemba kwa wanaosema Rais Magufuli Dikteta (+ video )

on

Hii ni kauli ya waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba kuhusu wale wanaoendelea kusema Rais Magufuli ni dikteta.

Amesema ‘Rais wetu ni mtu anaeishi kwa kufata sheria na ni mtu anaependa haki kwahiyo wanaopenda kutenda uovu wanapokutana na sheria ndio hao utasikia wanalialia

‘Niwaambie tu kwamba kama hawawajui Madikteta waende upya wafatilie Dikteta anakuaje, nikwambie hata kwa maeneo ambayo tumeona yakiwa na viashiria vya kidikteta kwanza mtu kusema tu huyu ni Dikteta unakua ulishakimbia kwenye hiyo nchi’ – Mwigulu

Hapa Tanzania wanaosema hivyo wako na soda zao, wengine wako disco na ratiba zao za kila leo wanafurahia maisha huku wanasema hivyo, utawala wa sheria Tanzania unaendelea na Rais hajatoa hukumu hata moja lakini kwa maeneo yaliyowahi kuwa na Madikteta kuna watu waliwahi kunyongwa uwanja wa taifa na anaesimamia ni kiongozi yeye mwenyewe yani hawajapitia Mahakama, yeye mwenyewe ndio anaamuru wanyongwe‘ – Mwigulu Nchemba

Kutazama zaidi aliyoyasema Mwigulu Nchemba unaweza kuyatazama kwenye hii video hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments