Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Sababu za Giroud kumzawadia goli David Luiz dhidi ya Liverpool

on

Jumapili ya May 6 2018 Chelsea walikuwa wenyeji wa Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu England wakati huu ambao Chelsea wanapambania nafasi ya kucheza michuano ya UEFA Champions League msimu ujao kwani kwa sasa wapo nafasi ya 5 nyuma ya Tottenham.

Chelsea wakiwa nyumbani walifanikiwa kufufua matumaini ya kumaliza Ligi wakiwa TOP 4 kufuatia ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Oliver Giroud dakika ya 32, Giroud baada ya kufunga goli alikimbia hadi benchi kwenda kumkumbatia mchezaji mwezake David Luiz.

Baada ya game Giroud alisema goli hilo amelitoa kwa Luiz kwa heshima na kumtakia kheri”David Luiz ni rafiki mzuri hivyo nilikuwa na furaha goli langu nililofunga kumzawadia yeye kwa kwenda kushangilia nae kwa sababu najua anapitia kipindi kigumu sana kwa sasa na naamini atarejea uwanjani salama”>>> Oliver Giroud

VIDEO: Emmanuel Okwi hawezi kupata presha kwa rekodi ya Tambwe VPL

Soma na hizi

Tupia Comments