Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Mtanzania Abdi Banda ametwaa tuzo katika club yake Afrika Kusini leo

on

Beki wa kati wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza soka la kulipwa katika club ya Baroka FC ya Afrika Kusini Abdi Banda leo amerudi tena kwenye headlines baada ya kufanikiwa kutangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi April wa club ya Baroka FC.

Banda leo amefanikiwa kutangazwa mchezaji bora wa Baroka FC ambapo hivi karibuni aliifungiwa magoli mawili timu yake katika mchezo dhidi ya Bloemfontein Celtic, Banda ametangazwa mshindi wa tuzo hiyo na kupewa hundi ya rand 5000 ambazo ni zaidi ya Tsh laki tisa.

Kama hufahamu Banda amekuwa na wakati mzuri na Baroka FC kutokana na kufanikiwa kucheza jumla ya mechi 31, 27 za Ligi na nne za mashindano mengine na kati ya game 31 alizocheza ni mechi moja pekee dhidi ya Free State February 3 2018 ndio alicheza kwa dakika 63 ila game nyingine zote alicheza kwa dakika zote 90, hadi sasa ameoneshwa jumla ya kadi tatu za njano.

VIDEO: Emmanuel Okwi hawezi kupata presha kwa rekodi ya Tambwe VPL

Soma na hizi

Tupia Comments