Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Uwezekano wa Kinda huyu wa Brazil kuziba nafasi ya Sanchez Arsenal

on

Mojawapo ya stori kubwa katika klabu ya Arsenal kwa sasa ni Sanchez pamoja na Ozil kuwa katika harakati za kutaka kuondoka klabuni hapo, ripoti iliyotoka katika gazeti la Daily Mail zinasema uwezekano wa Arsenal kumsajili mshambuliaji wa pembeni wa Bordeaux, Malcom (20) umeongezeka baada ya Manchester United na Tottenham kujiondoa katika kinyang’anyiro cha kumsajili.

Malcom, ambaye ana uraia wa Brazil, anatarajiwa kuwa mrithi sahihi wa Alex Sanchez ambaye sasa ni dhahiri kuwa anaondoka Arsenal. Mkataba wa Sanchez umeingia katika miezi sita ya mwisho na amekataa kuingia kwenye majadiliano ya kuingia mkataba mpya.

Bordeaux wameweka wazi kuwa wanahitaji £45millioni/= ili wamwachie.

REKODI ALIYOIWEKA GUARDIOLA BAADA YA KUSHINDA TUZO YA KOCHA BORA WA MWEZI.

Soma na hizi

Tupia Comments