Mix

UMRI SIO ISHU: Mastaa 9 wa kike walioolewa na wanaume wenye umri mdogo

on

tory kubwa ambayo ilikuwa gumzo mitandaoni mapema mwezi May ni kuhusu Brigitte Trogneux ambaye ni mke wa Rais wa sasa wa Ufaransa, Emmanuel Macron ambaye ana miaka 64 akimzidi kwa miaka 25 mumewe mwenye miaka 39.

Mbali na Brigitte Trogneux ambaye alikuwa mwalim wa Rais huyo wapo mastaa wengine wa kike ambao wameolewa na wanaume wenye umri mdogo.

Tina Turner – Mwimbaji, muigizaji na mwandishi wa Marekani

Baada ya kudumu kwenye uchumba kwa miaka 25 hatimaye mwaka 2013, Tina Turneralifunga ndoa na Erwin Bach. Wakati wanafunga ndoa Tina alikuwa na umri wa miaka 74 na mumewe alikuwa na umri wa miaka 58.

Muigizaji Mary Tyler Moore alifunga ndoa na Robert Levine mwaka 1983 ambapo Maryalikuwa na umri wa miaka 47 na Robert alikuwa na umri wa miaka 29.

Mary Tyler Moore – Muigizaji wa Marekani

Demi Moore – Mwandishi wa nyimbo, Mwanamitindo na Muigizaji wa Marekani

 

Mwaka 2005 Demi Moore alifunga ndoa na Aston Kutcher wakati akiwa na umri wa miaka 43 na mwanaume alikuwa na umri wa miaka 27. Ndoa hiyo ilidumu hadi mwaka 2013.

oan Collins – Mwandishi wa Makala na muigizaji wa Uingereza

Joan Collins na Percy Gibson walifunga ndoa 2002 wakati huo mwanamke alikuwa na umri wa miaka 69 na mwanaume alikuwa na umri wa miaka 37.

Elizabeth Taylor – Mfanyabiashara na muigizaji mwenye asili ya Marekani na Uingereza

Elizabeth Taylor alifunga ndoa na Larry Fortensky mwaka 1991 akiwa na miaka 59 na mwanaue alikuwa na umri wa miaka 39. Ndoa hiyo ilidumu hadi mwaka 1996.

Carol Burnett – Muigizaji wa Marekani, Mchekeshaji na mwimbaji

Ndoa ya Carol Burnett na Brian Miller ilifungwa mwaka 2001 wakati huo mwanamke alikuwa na umri wa miaka 68 na mwanaume alikuwa na umri wa miaka 45.

Ivana Trump – Mwanamitindo na mfanyabiashara mwenye asili ya Marekani na Czech

Ivana Trump aliolewa na Rossano Rubicondi mwaka 2008 akiwa na umri wa miaka 59 na mumewe miaka 36. Ndoa hiyo haikufikisha hata mwaka mmoja. Ivana aliolewa mara tatu kabla huku ndoa yake ya pili ikiwa na mjasiriamali Donald Trump ambaye ndiye Rais wa sasa wa Marekani.

Norma Shearer – Muigizaji mwenye asili ya Canada na Marekani.

Norma Shearer alifunga ndoa na Martin Arrougé mwaka 1948 akiwa na umri wa miaka 46 na mwanaume akiwa na miaka 26. Wawili hao walikuwa pamoja hadi mwanamke alipofariki mwaka 1983.

Edith Piaf – Mwimbaji wa Ufaransa

Edith Piaf aliolewa na Théo Sarapo mwaka 1962 akiwa na umri wa miaka 46 na mwanaume alikuwa na umri wa miaka 26. Walidumu katika ndoa hiyo kwa miaka miwili kabla ya mwanamke kufariki.

Soma na hizi

Tupia Comments