Mtu mmoja amewafyatulia risasi watu wawili na kupelekea mmoja kufariki na mwingine kujeruhiwa akiwalalamikia kumpigia kelele wakati watu hao walipokuwa kwenye mkesha wa harusi Dar.
Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kipolisi Ilala, David Mwambunga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo japo amekataa kuzungumzia suala hilo kwa kuwa yeye sio msemaji rasmi.
Majeruhi wa tukio hilo, Goodluck Madaraka amesema siku ya tukio walikuwa wakicheza muziki majira ya saa tano usiku ndipo jirani yao Lucas Muhabe alitoka na panga akiwafukuza kwamba wanampigia kelele, muda mfupi baadaye akarudi na bastola na kuanza kupiga risasi hewani ambapo moja ilimpata mpita njia Mahamudu Muhasi kichwani, akafariki.
Kaka wa marehemu amesema mdogo wake alikuwa akipita njia tu jirani na ilipo sherehe hiyo hivyo ameuawa lakini hakuhusika.
NIPASHE
Kuongezeka kwa ndoa za mikeka kumesababisha kuongezeka kwa talaka katika Mahakama Kuu Z’bar ambapo mwanaharakati wa Chama cha Wanahabari, Amina Talib amesema ndoa hizo ambazo zinafahamika pia kama ndoa za kukamatiwa zinaharibu mfumo mzima wa maisha.
Amina alisema katika Ripoti zilizotolewa na chama hicho, Mahakama za kadhi ambazo zimekuwa na majukumu ya kusikiliza kesi za ndoa na mirathi zimeelemewa na idadi kubwa ya maombi ya talaka huku watendaji wa Mahakama hiyo wakilaumu wananchi kutochukua hatua yoyote kunusuru hali hiyo.
Wazazi wametakiwa kuwalea watoto wao kwa maadili ili kukwepa vitendo vya ushawishi wa kuingia katika uhusiano wa kimapenzi kabla ya umri.
HABARI LEO
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Mary Nzuki amesema wanamshikilia mfanyabiashara Lucas Sasha kwa kosa la kumuua mpita njia Mahmoud Ally kwa kumpiga risasi maeneo ya Tabata Kisukulu wakati wa sherehe za Christmas.
Kwa mujibu wa maelezo aliyoyatoa Sasha amesema kuwa kulikuwa na kundi kubwa la vijana waliokuwa wanapita mbele ya nyumba yake hivyo akadhani kuwa amevamiwa na vibaka, akaamua kupiga risasi.
Kamanda Nzuki amesema mfanyabiashara huyo anamiliki bastola hiyo kihalali, kwa sasa Polisi wanamshikilia kwa ajili ya uchunguzi wa tukio hilo
JAMBO LEO
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Victor Mwambalaswa amesema kuwa yupo tayari kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti wa Kamati hiyo kwa kuwa anatambua maana ya uwajibikaji.
Mwambalaswa amesema anayaheshimu maazimio ya Bunge hivyo ni lazima akubaliane nayo kwa kuwa yeye alikuwa mmoja ya waliopitisha maazimio hayo.
Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Naibu Spika Job Ndugai kutoa tamko kwamba washukiwa wote wa sakata la uchotwaji wa pesa za Escrow wahakikishe wanaachia ngazi wiki mbili kabla ya Kikao cha Bunge kuanza hapo Januari 27.
TANZANIA DAIMA
Mtu mmoja asiyefahamika amekufa kwa kujilipua bomu alilokuwa amelenga kuwalipua Polisi waliokuwa katika doria Songea siku ya Krismasi.
Kaimu Mkurugenzi wa makosa ya jinai nchini, Naibu Kamishna Diwani Athumani amesema tukio hilo lilitokea juzi Desemba 25 majira ya saa moja usiku ambapo Polisi walipitwa na gari dogo ambalo liliegeshwa mbele yao na muda mfupi wakasikia kishindo cha mlipuko.
Watu kadhaa walionekana wakiuchukua mwili wa mtu huyo aliyejeruhiwa ili waupakie kwenye gari iliyokuwa imesimama mbele ya gari ya Polisi, baada ya kuwaona Polisi waliuacha mwili wa mtu huyo na kukimbia.
Katika tukio hilo Polisi wawili walijeruhiwa lakini hali zao zinaendelea vizuri huku upelelezi ukiendelea kubaini wahusika wa tukio pamoja na lengo lao kwa kuwa mazingira yanaonyesha kuwa lengo lilikuwa kuwadhuru Askari Polisi hao waliokuwa doria.
TANZANIA DAIMA
Wengi tumezoea kwamba kila anayehudhuria sherehe kubwa za Kitaifa na kupita red carpet lazima awe amevalia vizuri kuendana na sherehe husika.
Story ni kwamba mama mzazi wa Naibu Rais wa Kenya, William Ruto ambaye jina lake Sarah Cheruiyot alihudhuria siku ya sherehe za maadhimisho ya Uhuru wa Kenya akiwa amevaa ndala au wengine huyaita malapa na akapita zake red carpet.
Story ni kama ilikuwa kubwa uwanja wa Nyayo ambapo sherehe za maadhimisho hayo zilifanyika, lakini wengine wanahisi kwamba huenda mama huyo alifanya hivyo kama njia ya kutangaza bidhaa hiyo.
Nakuhakikishia kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook