Michezo

Dakika nne zimewatosha Man United kupindua matokeo kwa Juventus

on

Baada ya kupoteza game yao ya kwanza kwa goli 1-0 Man United katika uwanja wao wa nyumbani wa Old Trafford dhidi ya Juventus, usiku wa November 7 2018 walikuwa ugenini Italia kucheza game ya marudiano dhidi ya Juventus game ya Kundi H.

Man United wakiwa katika uwanja wa Juventus wamehakikisha wanapata ushindi na kuvunja rekodi ya staa wa Juventus Cristiano Ronaldo ambaye alikuwa hajawahi kufungwa dhidi ya Man United toka alipoihama club hiyo mwaka 2009 na kujiunga na Real Madrid wakati huo, Juventus leo wamepoteza kwa magoli 2-1 wakiwa nyumbani.

Kipigo cha Juventus kimewashangaza wengi licha ya wengi kuamini kuwa kwa sasa Juventus wana timu bora zaidi ya Man United ambayo indaiwa kwa sasa kuwa na mgawanyiko ndani kwa kuwa na makundi yasio kuwa na msingi kutokana na mgogoro wa Pogba na Mourinho.

Juventus ndio walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 65 kupitia kwa staa wao Cristiano Ronaldo ambaye alipiga volley na mpira kuzama wavuni, tukiwa wengi tunaamini mchezo utamalizika kwa Juventus kupata ushindi wa goli 1-0, dakika ya 86 Juan Mata akabadili matokeo kwa kufunga goli la kusawazisha kabla ya dakika ya 90 Juventus kupitia kwa ย Alex Sandro kujifunga na kupoteza mchezo huo.

Licha ya kipigo hicho Juventus wanaendelea kuongoza Kundi H kwa kuwa na jumla ya point 9 walizozivuna katika mchezo mitatu ya awali, wakati Man United wamefikisha point saba na kuwa nafasi ya pili, Valencia nafasi ya tatu kwa kuwa na point 5, Young Boys wakishika mkia kwa kuwa point 1.

Hakuna anayemkuta Samatta kwa sasa Jupiter Pro League 2018/19

Soma na hizi

Tupia Comments