AyoTV

Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake

on

Moja kati ya habari kubwa zilizoanzia siku ya Jumamosi ya February 16 ni kuhusiana na shabiki wa Yanga anayefahamika kwa jina la Jimmy Kindoki kuanza kulia baada ya kuona timu yake ya Yanga imefungwa 1-0 dhidi ya Simba na baadae kugundulika kuwa alibet mke wake yaani aliicheza kamali akamuweka dau mke wake.

Jimmy Kindoki alibet na rafiki yake Justine Kessy ambaye ni shabiki wa Simba kuwa Simba itafungwa na Yanga na kama Simba itaifunga Yanga basi aende akamchukue mke wake (JIMMY Kindoki) na Justine Kessy alimuahidi Jimmy Kindoki kama Yanga itamfunga Simba basi atatoa mshahara wake wa mwezi na kumpa Jimmy Kindoki.

Sasa Yanga imefungwa na Justine Kessy alipaswa kupewa mke wa Jimmy Kindoko, Jimmy alikuwa analia na kuomba msamaha tu, leo kwenye AyoTV imempata katika EXCLUSIVE JIMMY Kindoki ambaye alibet mke wake ameeleza kuwa alikutana na kocha wa Yanga Mwinyi Zahera siku moja kabla ya mechi na alimwambia kuwa Yanga lazima imfunge Simba, hivyo akaamini kwa kiwango kikubwa.

Justine Kessy amekubali kumsamehe Jimmy Kindoki lakini kwa sharti moja la kutaka alipwe Tsh laki tano kama fidia, kwa upande wa familia mke wa Jimmy Kindoki ameondoka nyumbani na imepangwa kuwa watamuweka kikao Jumamosi hii na kuamua nini cha kufanya kutokana na kosa alilolifanya.

Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera kataja walichozidiwa wachezaji wake na Simba

Soma na hizi

Tupia Comments