Tangaza Hapa Ad

Mix

Taarifa nyingine kuhusu ajali ya Toyota Noah Singida, hii ni kauli ya Polisi.

on

latestHizi ni dakika chache tuzitumie kusikiliza alichokisema Kamanda wa polisi mkoa wa Singida ACP.Geofrey Kamwela kuhusu ajali iliyotokea leo asubuhi ambayo imehusisha gari aina ya Toyota Noah na Scania lori ambayo taarifa inasemekana yaligongana uso kwa uso na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 10 na majeruhi.

singidaaKamanda anaanza kwa kusema>>’Ni asubuhi ya leo saa 2 kule Isuna katika wilaya ya Ikungi mkoani Singida, ajali imehusisha magari mawili moja aina ya Noah na nyingine ni Scania lori,yamegongana uso kwa uso na kusababisha vifo vya watu 13′

‘Inavyoonekana kuna uzembe fulani  ulitokea pale kutokana na kwamba magari haya yamegongana yakiwa upande mmoja wa barabara kuu ya kutoka Singida Dodoma baada ya kugongana ile Toyota Noah ilisukumwa mpaka nje ya barabara halafu ile lori ikaenda hadi mbele ikasimama kisha Dereva na Utingo wakakimbia’

‘Mpaka sasa hivi Dereva wa Lori hilo na Utingo wake tunawatafuta kwa ajili ya kuhojiwa kutupa taarifa zaidi,kuhusu wale waliokuwa kwenye Noah dereva pengine na kondakta na abiria ndo hao wamepoteza uhai  japo tuna mtu ambaye yeye alinusurika mmoja tu kwen ye hiyo Noah bado hatujaweza kumhoji maiti wote walichukuliwa asubuhi wakapelekwa kwenye Hospital ya Mkoa wa Singida.

Msikilize Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida kwa kubonyeza play.

Tupia Comments

Advertisement