Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Michezo

Chirwa awashinda Nyoni na Ajib… sababu ziko hapa

on

Ni habari inayomuhusu Obrey Chirwa, Mchezaji staa kutoka timu ya Dar es salaam Young Africans a.k.a Yanga ambapo leo November 9 2017 Chirwa ametangazwa Mshindi wa Tuzo ambayo alikua akiiwania yeye na wakali wengine wawili.

Chirwa ametangazwa kuwa Mchezaji bora wa October kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara ambapo atapewa Tsh. Milioni 1 kama zawadi baada ya kuwashinda Erasto Nyoni wa Simba na Mchezaji mwenzake wa Yanga Ibrahim Ajib.

Ameshinda tuzo hiyo kwa kuiwezesha Yanga ndani ya mwezi October pekee kuvuna point 7 kwenye game zao 3 walizocheza na kuisogeza Yanga kwenye nafasi ya pili kutoka ya 6 mwezi September, pia ameisaidia Yanga kupata ushindi wa goli 2-1 vs Kagera Sugar huku akifunga moja na kutoa pasi iliyozaa goli kwenye ushindi huo.

Kwenye ushindi wa magoli manne kwa bila vs Stand United Obrey Chirwa alifunga goli moja na kutoa pasi ya goli la mwisho na pia aliinusuru Yanga vs Simba kwa kuisawazishia goli kwenye sare ya 1-1 kwenye game iliyochezwa uwanja wa Uhuru Dar es salaam.

BREAKING: Mbwana Samatta katisha tena rekodi za Afrika, bonyeza play hapa chini kufahamu zaidi

UNAZITAKA BREAKING NEWS FASTAFASTA? Jiunge na Reporter wako Millard Ayo kwa kubonyeza kifuatacho SUBSCRIBE >>> YOUTUBE , APP YA MILLARD AYO, FACEBOOK , INSTAGRAM

Soma na hizi

Tupia Comments