PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Michezo

Ureno na Argentina wote safari zimewakuta

on

Baada ya kuchezwa kwa game ya kwanza ya hatua ya 16 bora kati ya Ufaransa dhidi ya Argentina na kushuhudia Lionel Messi na Argentina yake wakiyaaga mashindano hayo kwa kipigo cha magoli 4-3.

 

Usiku wa June 30 ilichezwa game ya pili ya hatua ya 16 bora kwa kuzikutanisha timu za Ureno dhidi ya Uruguay, huku dunia ikiwa na shauku ya kutaka kujua Cristiano Ronaldo ataifanyia nini Ureno baada ya Messi kushindwa kuisaidia Argentina isiondoke katika mashindano hayo.

Ronaldo na Messi wote wamekumbwa na bahati mbaya leo kwani Edinson Cavani amepeleka majonzi kwa wareno kama alivyofanya Mbappe kwa Argentina, Cavani ameifungia Uruguay magoli mawili dakika ya 7 na 62 katika ushindi wa 2-1.

Goli la pili la Uruguay lilikuja ikiwa ni dakika 7 zimepita toka Pepe aisawazishie Ureno kwa kichwa, licha ya Ureno kumiliki mpira kwa asilimia 67 kwa 33 lakini hawakuweza kupata matokeo katika mchezo huo, kocha wa Uruguay Oscar Tabarezย anaipeleka Uruguay robo fainali akiwa ndio kocha mkongwe kufundisha timu katika mashindano hayo akiwa kadumu nayo toka 1990.

Haji Manara kapenda usiku wa VPL ila kafunguka wasiwasi wake

Soma na hizi

Tupia Comments