Michezo

Kiasi cha Pesa alichovuna Mourinho na wasaidizi wake kutoka Man United

on

Baada ya kupita takribani miezi miwili toka kocha Jose Mourinho afutwe kazi na club ya Man United na nafasi yake kupewa kocha wa mpito Ole Gunnar Solskjaer kutokana na mwenendo mbovu, leo imethibitika kuwa Man United iliwalipa mamilioni ya Tsh Jose Mourinho na wasaidizi wake.

Kwa kawaida kocha akifutwa kazi kama bado ana mkataba hiyo ni sawa na club imevunja mkataba nae, hivyo baada ya Jose Mourinho na wasaidizi wake kufutwa kazi inadaiwa kuwa walilipwa zaidi ya Tsh Bilioni 58. kama fidia ya kuvunjwa mkataba wake na uongozi wa Man United.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Jose Mourinho alijiunga na Man United 2016 kama kocha Mkuu akifutwa kazi Chelsea 2015, hadi anaondoka Man United December 2018 alikuwa amekusanya point 26 katika Ligi Kuu akiwa kaiongoza club hiyo katika michezo 17.

Imeshinda Simba SC tabu kaipata JB wakati wa kutoka

 

Soma na hizi

Tupia Comments