PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Michezo

Refa tajiri ndio ataamua hatma ya England vs Sweden

on

Bjorn Kuipers ambaye anatajwa katika list ya kuwa refa tajiri zaidi duniani leo Julya 5 2018 FIFA wamemtangaza rasmi kama ndio muamuzi atakayechezesha mchezo wa robo fainali ya England dhidi ya Sweden.

Bjorn Kuipers ambaye aliingia rasmi katika kazi ya urefa 2002 akifuata nyayo za baba yake ambaye alikuwa refa pia, alianza kupata mashavu ya kuchezesha mechi za FIFA mwaka 2006 kutokana na uwezo wake aliouonesha.

Utajiri wa refa Bjorn Kuipers kufikia mwaka 2016 ulikuwa unatajwa kufikia pound milioni 11.5 na anatajwa kuingiza kiasi cha pound kati ya milioni 2 hadi 3 kwa mwaka, hadi sasa katika World Cup Bjorn Kuipers amechezesha jumla ya game 3 na kutoa kadi nane za njano.

Rekodi ya Bjorn Kuipers akichezesha Ligi Kuu Uholanzi.

Haji Manara kapenda usiku wa VPL ila kafunguka wasiwasi wake

Soma na hizi

Tupia Comments