PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

Michezo

Chelsea wameipa baraka rasmi Man United ya kukaa TOP 4

on

February 10 ilikuwa ni siku ya Big Game kwa England kwani club ya Man City ilikuwa inaikaribisha rasmi Chelsea katika uwanja wa Etihad kucheza game yake ya 26 ya Ligi Kuu England, game hiyo inatwajwa kuwa muhimu sana kwa timu zote mbili kutokana na zote zinahitaji point.

Chelsea ilikuwa inahitaji point ili irudi TOP 4 na kuishusha Man United wakati Man City ilikuwa inahitaji point ili kurudi nafasi ya pili katika msimamo wa EPL, nakujiweka nafasi nzuri ya kutetea taji hilo kwa karibu zaidi na kuipa presha Liverpool iliyopo nafasi ya kwanza.

Kwa bahati mbaya Chelsea ameruhusu kipigo kikubwa cha kufungwa kwa magoli 6-0, magoli ya Man City yakifungwa na Raheem Sterling aliyefunga magoli mawili dakika ya 4 na 80, Sergio Aguero aliyefunga hat-trick dakika ya 13, 19 na dakika ya 56 kwa mkwaju wa penati na Gundogan dakika ya 25.

Kipigo hicho kwa Chelsea kinaifanya Man United kujihakikishia nafasi ya kuwa TOP 4 jumla, kwani jana baada ya Man United kuingia TOP 4, ilikuwa inasubiria na kuiombea Chelsea ipoteze mchezo wake dhidi ya Man City, ili wao Man United wasalie TOP 4.

“Tunashindana na timu zenye nguvu, aliyetoa assist Alexandria kanunuliwa Bilioni 10”-MO Dewji

Soma na hizi

Tupia Comments