PremierBet Ad
Asas Dairies Ad
NBC Ad

AyoTV

Tido Mhando na DC Jokate Mwegelo wamezindua tuzo za SZIFF 2019 leo

on

Baada ya kufanyika kwa mara ya kwanza kwa mafanikio msimu uliopita wa tuzo za Sinema Zetu International Film Festival, msimu wa 2019 umezinduliwa leo na mabadiliko chanya yametangazwa.

Waratibu wa tuzo za SZIFF 2019, Azam TV kupitia CEO wao Tido Mhando wametaja kuwa moja kati ya maboresho waliyoyatangaza leo ni pamoja na vipengele, ambapo safari hii itakuwa vipengele 24 kutoka 19 vya msimu uliopita.

SZIFF pia imemtangaza Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo ambaye alikuwa sehemu ya tukio hilo, kuwa ndio mlezi rasmi wa tuzo hizo, kilele cha tuzo za Sinema Zetu International Film Festival zitatolewa February 23 2019.

EXCLUSIVE: Licha ya kuwa na pesa na ustaa, hii ndio Sababu inayomfanya Samatta asiringe

Soma na hizi

Tupia Comments