Top Stories

Maagizo ya Mbarawa kwa Shirika la reli juu ya ajali ya kigoma

on

Leo June 11, 2018 Nakusogezea stori kutoka kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ambapo ametoa miezi 3 kwa Shirika la Reli Tanzania kuhakikisha linaweka alama (barrier) katika kila eneo la makutano ya barabara na reli.

Prof. Mbarawa ametoa amri hiyo ikiwa ni takribani wiki moja tangu ilipotokea ajali ya basi la abiria kugongana na treni Gungu mkoani Kigoma, ambapo ilisababisha vifo vya watu 10.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Prof. Mbarawa amesema suala la usalama katika reli ni muhimu hasa katika uwekaji wa barrier.

“Hivyo Maria miezi mitatu kuanzia leo kila kwenye makutano ya reli na barabara kuwekwe barrier na waajiriwe watu, lengo ni kulinda maisha ya Watanzania wenzetu, “ amesema Mbarawa

Prof. Mbarawa amesema linaweza kuonekana ni jambo dogo lakini litaokoa maisha ya watu wengi.

Maagizo aliyotoa Naibu Waziri Kilimo Dr. Mwanjelwa katika ziara Njombe

Soma na hizi

Tupia Comments