Tangaza Hapa Ad

HekaHeka

HEKAHEKA: Geah Habib ameifuatilia ishu ya mtoto aliyepigwa risasi na polisi DSM

on

Leo December 5 2016 Heka Heka ndani ya Clouds FM  ya Geah Habibu imeifuatilia kwa ukaribu ishu ya mtoto aliyepigwa risasi na polisi jijini Dar es salaam

Geah amezungumza na mtoto huyo ambapo amesema………>>>tulikuwa tumetoka shule ya msingi ya zanaki kuchukua vyeti wakati tunarudi, ghafla nikasikia kama tairi limepasuka, kuangalia mbele nikaona askari mwenye silaha akapiga chini, ya pili ikaenda kwenye gari, ya tatu ikanipata nikawa nimesikia ganzi, nikarudi nyuma nikaomba msaada

‘Daktari alituambia hiyo risasi ipo katikati ya kibofu cha mkojo na utumbo mkubwa na eneo hilo pia kuna ule mshipa wa kupeleka damu kwenye moyo kwa hiyo risasi imeenda pale imetulia, tukamuuliza aina madhara akasema haina madhara kwa sababu imekwenda pale imetulia wakisema waitoe italeta matatizo mengine kwa sababu sehemu zote zile ni laini’-Shangazi wa mtoto

‘Polisi wamekuja wanaonana na mtoto hawaonani na sisi hospitali, alinipigia simu polisi wanasema wameshashughulikia ile bili ya hospitali kwa hiyo tukamchukue yule mtoto, polisi aliyempiga risasi wamesema hawezi kuonekana kwa sababu ya usalama wake, tumekwenda polisi tumeona faili lake lipo’;-Shangazi wa mtoto

risasi

Bonyeza play hapa chini kusikiliza full stori

ULIKOSA? Dakika 12 za JK Comedian mbele ya Waziri Mwigulu na Charles Mwijage, Bonyeza play hapa chini kutazama 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement