Tangaza Hapa Ad

AyoTV

VIDEO: Waziri Nchemba alipokutana na kijana aliyegongwa na gari la polisi na kupooza mwili

on

Kijana ALLY MKINGI (23) wa kijiji cha KIFINGA kata ya RUAHA ambaye June mwaka 2014 aligongwa na gari la Polisi lililokuwa linaikwepa pikipiki iliyoingia ghafla barabarani, likaacha njia na kupinduka mara kadhaa na kumkuta kijana huyu aliyekuwa kando kabisa ya barabara akitembea kwa miguu.

Ally ameumia sana na kupooza kuanzia kifuani mpaka chini na bahati mbaya sana kukosa uwezo na msaada zaidi kulala ndani tu kwa zaidi ya miaka 2 na mwili wake ukaanza kuharibika vibaya kwa vidonda vikubwa, Pamoja na jitihada kubwa za kumtibia lakini ripoti ya madaktari bingwa wa Hospitali ya Muhimbili (MOI) wametuambia ALLY hataweza kurudi kwenye hali yake ya kawaida kwani muda umepita sana hivyo andelee kumtibiwa vidonda hivyo.

Vidonda hivyo vimesababishwa na kulala sana ndani na kujisaidia hapohapo kwa kutumia mipira hivyo kutengeneza unyevunyevu. Kupitia jitihada za mbunge wa mikumi Joseph Haule “Prof J” kumsaidia kijana huyo kwa vitu mbalimbali Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mwiguru Nchemba ameombwa na Prof J kumsaidia kijana huyo naye akakubali kumsaidia gharama za matibabu ili atibiwe na siku ya ijumaa atakutana na daktar aliyekuwa anamtibu, kijana Ally ana Mke na Mtoto mmoja.

VIDEO: Mbunge wa kilombero alivyohoji mbele Waziri Nchemba kwanini hapigiwi saluti na polisi, Bonyeza play hapa chini 

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement