fB insta twitter

Alichoandika Manara baada ya Ubingwa wa Yanga na kuhusu FIFA

on

Saa kadhaa baada ya Yanga kukabidhiwa kombe kama Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara msimu wa mwaka 2016 – 2017, Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano SimbaHaji Manara ameamua kuwakumbusha Yanga kwa kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

May 20, 2017 Haji Manara ametumia ukurasa wake kuwaeleza Yanga kuwa Simbahawajakata tamaa kuhusu kudai Point zao 3 walizokuwa wamepewa na baadae kupokonywa kwenye ishu ya mchezaji aliyecheza akiwa na kadi tatu za njano, huku akisisitiza kuwa Yanga watalipeleka Kombe msimbazi kwa magoti…

..>>>”Last week nilipowapongeza Yanga kwa ushindi na kuwaambia mapambano yanaendelea,sijui kama tulielewana!! Bila shaka sasa mmenielewa,,soon tutapewa haki yetu,MWANA KULITAKA,MWANA KULIPEWA.

“Hivi unadhani FIFA wana figisu guys? kadi tatu za njano ni kukosa game inayofuata tu no way out!! ukizingatia reppti za mwamuzi na kamisaa na bodi inayosimamia ligi, sasa mjiandae kisaikolojia kulileta kombe kwa magoti! @Yangasc @simbasctanzania” – Haji Manara

Viwili vya imani za kishirikina vilivyoshangaza watu Live MbaoFC vs Yanga leo (+video)

Soma na hizi

Tupia Comments