Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Top Stories

Rais Magufuli amefanya uteuzi huu leo

on

Leo January 11, 2018 nimepokea taarifa toka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi, amemteua Alphayo Kidata kuwa Balozi.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi ameeleza kuwa uteuzi wa Alphayo Kidata umeanza Januari 10, 2018. Kabla ya uteuzi huo, Alphayo Kidata alikuwa Katibu Mkuu, Ikulu.

Rais Magufuli pia amemteua Meja Jenerali Mstaafu Simon Mumwi kuwa Balozi.

Mabalozi hawa wateule watapangiwa vituo vya kazi na kuapishwa baada ya taratibu kukamilika.

BREAKING: LOWASSA AMFATA MAGUFULI IKULU

JPM IKULU: “LOWASSA HAKUWAHI KUNITUKANA HATA SIKU MOJA”

Soma na hizi

Tupia Comments