Fastjet

Azam FC hatari, hiki hapa ndicho kilichoikuta Ruvu Shooting leo Chamazi

Wakati Simba ikibanwa mbavu, mabingwa watetezi wa ligi hiyo Azam FC leo walijitupa dimbani kuendeleza harakati za utetezi wa ubingwa wa kwanza wa Vodacom Premier League. AZAM FC imekaa kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuichapa mabao 2-0 Ruvu Shooting ya Pwani Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Azam FC walikwenda kupumzika wakiwa wanaongoza bao 1-0 lililofungwa na Mrundi, Didier Kavumbangu, ambalo hilo linakuwa bao lake la tatu msimu baada ya kufunga mawili katika ushindi wa 3-0 kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Polisi Moro. Kavumbangu alifunga bao hilo dakika ya 40, baada ya kuuwahi mpira uliopanguliwa na kipa wa Ruvu, Abdallah Abdallah kufutia shuti la Kipre Tchetche aliyeungaisha krosi maridadi ya Shomary Kapombe. Kipindi cha pili, kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog alianza na mabadiliko akimpumzisha beki Kapombe aliyeumia na nafasi yake ikichukuliwa na Erasto Nyoni. Kavumbagu aliwainua vitini tena mashabiki wa timu ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa dakika ya 50 baada yakufunga bao la pili kwa kichwa akimalizia krosi ya Himi Mao Mkami. Salum Abubakar ‘ Sure Boy’ aliinyima Azam FC bao la tatu baada ya kushindwa kuunganisha krosi nzuri ya Kavumbangu dakika ya 70. Dakika ya 75, Kavumbangu alipata nafasi nzuri ya kufunga hat...
Read More »

Fiestani Songea September 26 2014!!

Fiesta music tour ilifanyika kwa mara ya kwanza 105.8 Songea na kuhudhuriwa na maelfu ya vijana ambao walishuhudia kazi za wakali kama Mr. Blue, Linah, Rachel Mapenzi, Madee, Nay wa Mitego, Stamina, T.I.D, Linex, ni show ambayo imefanyika kwa mara...
Read More »

Magazeti ya leo Jumamosi September 27 2014

Kama kawaida millardayo.com inakupa vichwa vya habari vya magazeti yote ya kila siku. Leo pia kuna headline mpya kwenye magazeti mbalimbali. Chukua muda wako kupitia kila kilichoandikwa kwenye kurasa za mbele za magazeti ya leo. Ni halali yako kupata kila...
Read More »
Scroll To Top