Tangaza Hapa Ad

Michezo

Uliokuwa mpango wa Real Madrid kuhusu Pep Gurdiola

on

Kuna baadhi ya vitu ni nadra sana kutazamiwa vinaweza kutokea katika soka japokuwa wakati mwingine hutokea, mara chache kuona vilabu vyenye upinzani vikiuziana wachezaji walio na mikataba nao, hii imeripotiwa na moja ya kituo cha radio Hispania Cadena Ser kuwa Real Madrid walimuhitaji Pep Guardiola.

Nahodha na kocha huyo  wa zamani wa FC Barcelona alihitajika na Real Madrid November 2015 ili arithi nafasi ya kocha wa Real Madrid wa wakati huo Rafael Benitez, kama mpango huo ungefanikiwa basi ungeshangaza wengi kutokana na historia ya Pep Guardiola kuinyanyasa Real Madrid akiwa kocha na mchezaji katika klabu hiyo.

Hata hivyo mpango huo haukufanikiwa uliokuwa unfanywa na Rais wa Real Madrid Fiorentino Perez na Real Madrid waliamua kumfuta kazi kocha Rafael Benitez January 2016 na nafasi yake akapewa mkongwe wa klabu hiyo Zinedine Zidane.

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement