Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Top Stories

Uteuzi wa kwanza alioufanya Rais Magufuli 2018 katika Baraza la Mawaziri

on

Leo January 6, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi katika Wizara ya Madini ambapo amemteua Doto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya mawasiliano ya Rais Ikulu, Doto Mashaka Biteko ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe na  alikuwa Mwenyekiti wa kamati ya muda iliyochunguza madini ya Tanzanite.

Kufuatia uteuzi huu alioufanya President Magufuki leo, Wizara ya Madini sasa itakuwa na Waziri na Manaibu waziri wawili.

Rais Magufuli amefanya uteuzi huu kwa lengo la kuongeza nguvu kutokana na wingi wa majukumu katika Wizara ya Madini.

Doto Mashaka Biteko ataapishwa Jumatatu tarehe  January 8, 2018 saa 3:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.

ULIPITWA NA HII YA BARUA ALIYOIPOKEA LEO JPMA TOKA KWA RAIS MUSEVENI

GOOD NEWS: JPM ATANGAZA KUTOA TSH BILIONI 200

Soma na hizi

Tupia Comments