Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Top Stories

Bwana harusi kizimbani kwa namna rafiki zake walivyosherekea harusi yake

on

Polisi nchini Israel wanamshikilia mwanaume mmoja ambaye anatajwa kuwa bwana harusi baada ya kusambaa mitandaoni kwa video ya jinsi rafiki zake walivyosherehekea harusi yake.

Inaelezwa kuwa video hiyo ilionesha rafiki zake hao siku ya harusi yake wakiwa wamevaa nguo nyeusi na vinyago usoni kisha kupita kijijini hapo wakipiga risasi juu kwa madai ya kusherehekea harusi ya mwenzao.

 Mwanaume huyo ambaye anatajwa kuwa na umri kati ya miaka 20 na 30 alikamatwa jana na leo amefikishwa mahakamani kujibu kesi hiyo.

Raia na viongozi mbalimbali nchini humo wamezungumza na kusema kuwa walifikiri ni tukio la kigaidi lililokuwa likifanyika.

Serikali kuanza kuwapima UKIMWI na TB wanaume kwenye baa (Bar)

 

 

Soma na hizi

Tupia Comments