Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Mix

Picha ya Aika wa Navy Kenzo iliyotembea kwa spidi mitandaoni

on

Jioni ya January 19 2017 mwimbaji Aika wa kundi linalofanya muziki wa bongofleva Navy Kenzo ilianza kusambaa kwa nguvu kwa wanaofatilia habari za bongofleva na ni kutokana na picha hiyo kuhusisha Wasanii wengine wawili ambao waliwahi kutajwa kuwa na ugomvi.

Kundi la Pah One lilishaanza kupiga hatua kwenye bongofleva time hiyo likiundwa na Nahreel, Aika, Igwe na Ola, na wakatamba na single ya ‘Gheto’ lakini kwa bahati mbaya mwaka 2012 kundi likasambaratika.

Baada ya kusambaratika kwa kundi hili ndipo Aika na Nahreel waliamua kutengeneza kundi lao jipya la ‘Navy kenzo‘ huku Pah One wakibaki Ola na Igwe na baadae zilitoka stori kuwa Navykenzo na Pah One wana ugomvi ambapo kupitia Wikiend Chat Show ya CloudsTV pande hizi mbili zilikutanishwa na kumaliza tofauti zao.

Sasa kilichofanya Aika aziteke headlines za Internet ni kupost picha yake na Nahreel wakiwa pamoja na Pah One wote wakionekana kuwa na amani ndani ya studio za The Industry inayomilikiwa na Nahreel.

Taarifa zinasema inawezekana Navykenzo wakabeba jukumu la kuwasimamia Pah One kwenye label ya The Industry ambayo inawasimamia Wasanii wengine kama Rosaree, hii hapa chini ni moja nyimbo zao kabla kundi halijasambaratika.

Soma na hizi

Tupia Comments