Tangaza Hapa Ad

Michezo

PICHA: Baada ya kuwapiga hat-trick msimu uliopita, Tambwe kadhihirisha umahiri wake tena

on

Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea kwa michezo 5 kupigwa katika viwanja mbalimbali Tanzania, kwa upande wa Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu klabu ya Dar es Salaam Young Africans walishuka uwanja wa Uhuru Dar es Salaam kuwakaribisha Majimaji FC, hiyo ni baada ya kutoka suluhu na Ndanda FC katika uwanja wa Nangwanda.

img_0130

Katika mchezo huo wa tatu wa Ligi Kuu kwa Yanga wakiwa wameshinda mchezo mmoja dhidi ya African Lyon na kutoka suluhu na Ndanda FC, umemalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa goli 3-0, magoli ambayo yalifungwa na Deus Kaseke dakika ya 35 na Amissi Tambwe aliyefunga magoli mawili dakika 75 na 85 na kuendeleza rekodi yake dhidi ya Majimaji FC.

img_0127

Kama utakuwa unakumbuka mchezo wa mwisho wa Majimaji kucheza na Yanga Dar es Salaam January 21 2016 walikubali kipigo cha goli 5-0, huku Amissi Tambwe akipiga hat-trick lakini katika mchezo wa leo Tambwe ameishia kuzinyanyasa beki za Majimaji na kufunga magoli mawili pekee.

img_0122

Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu zilizochezwa leo Septemba 10 2016

GOAL AND HIGHLIGHTS: YANGA VS TP MAZEMBE JUNE 28 2016, FULL TIME 0-1

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement