Michezo

PICHA 3: Hassan Mwakinyo anaendelea kujifua England, Pambano March 23

on

Bondia mtanzania Hassan Mwakinyo bado anaendelea kujifua nchini England katika jiji la Liverpool kwa ajili ya maandalizi ya pambano lake la March 23 litakalofanyika nchini Kenya, Hassan Mwakinyo baada ya kufanya vizuri pasipo kuwa na udhamini alipewa udhamini na SportPesa kama balozi wao kwa ajili ya kumsaidia kupata mafunzo kwa ufanisi na vifaa.

Akiwa nchini England katika jiji la Liverpool Hassan Mwakinyo amepata fursa ya kufanya mazoezi au maandalizi ya pambano lake la March 23 kutoka kwa bondia wa England Tony Bellew ambaye nae amewahi kufanya vizuri katika mapambano mbalimbali, hivyo Mwakinyo sasa amepata fursa ya kuboresha kipaji chake.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri bondia Hassan Mwakinyo alijizolea umaarufu mkubwa mwezi September 2018 baada ya kumpiga bondia muingereza Sam Eggingtonkwa kumpiga Technical Knock Out  round ya 2 katika pambano la round 10.

Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake

Soma na hizi

Tupia Comments