Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Maamuzi ya mahakama juu ya kesi ya unyanyasaji wa watoto inayomkabili Brad Pitt

on

Muigizaji Brad pitt aliyekuwa mume wa  Angelina Jolie alikuwa na kesi iliyokuwa ikimkabili tangu September 2016 baada ya kusemekana alipishana maneno  na mtoto wake wa miaka 15, Maddox mpaka kufika hatua ya kumpiga.

Baada ya tukio hilo Brad amekuwa akifanyiwa uchunguzi mpaka Nov 9 2016 ambapo mahakama jijini Carlifonia imeamua kumfutia mashtaka hayo kwa kile kilichoelezwa kuwa amegundulika kuwa hana hatia.

Angelina Jolie, Brad Pitt na mwanao Maddox Jolie-Pitt

Uchunguzi uliofanywa na kitengo cha haki za watoto na familia kwa Brad, Angelina, watoto wao pamoja na watu wengine waliokuwa kwenye ndege na eneo ambalo inasemekana Brad alimdhuru mtoto huyo ulibaini hakumnyanyasa mtoto huyo kama ilivyodaiwa.

Angelina Jolie amekuwa akilalamika kuwa Brad Pitt amekuwa hana usimamizi mzuri kwa watoto wao, hivyo amekuwa na wasiwasi kumuachia asimamie malezi ya watoto wao.

Pamoja na hayo imeelezwa kuwa Angelina Jolie atabaki na  usimamizi mkuu kwa watoto wao sita Maddox, 15, Pax, 12, Zahara, 11, Shiloh, 10, na mapacha wawili, Knox na Vivienne  huku Brad Pitt akipangiwa siku za kwenda kuwasalimia.

MTV EMA kuichukua  tuzo kwa wizkid na kumpa Alikiba, BONYEZA PLAY HAPA CHINI

Nimekusogezea Full perfomance ya Alikiba kwenye Fiesta Dar 2016 kama hukuona unaweza kubonyeza Play>>>

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement