Biko Ad
MPTV Ad
Tangaza Hapa Ad

Habari za Mastaa

Kuna watu wamemtibua NANDY mpaka kaandika haya

on

Leo January 3, 2018 Kumekuwa na post kwenye mitandao ya kijamii kuhusu msanii Nandy kudaiwa kutoka kimapenzi na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, Nandy ameamua kuandika kwenye ukurasa wake wa Istagram kuhusu tuhuma hizo.

Nandy Kupitia ukurasa wake wa Isntagram ameandika kuwa. “Mtu akifanya mziki wake kwa amani bila drama kuna watu wanakuwa hawatosheki kabisa. hivi mimi ni kichaa mpaka kujiachia kama uyo msambaza habari anavyo sambaza!”

“Kwani suala la watu kusema na toka na boss wangu nalijua leo au nigeni kwangu sana mpaka nijiachie kwenda naye ma camp sijui ma club kama mnavosema???” – Nandy

“Embu tuwe na utu please kwa hiyo me nimekuwa wakuja kiasi kwamba mshamba kiasi nikashindwa kujificha na mashungi juu basi kama ni hivyoΒ  tumeshindwa kupishana kusafiri atangulie ndo nifuate,”– Nandy

“Kwani sijui hata kama ingekuwa ni kwa nia nzuriΒ  msingesema mnazani mambo ni marahisi kiasi hicho tupeane heshima kuna watu wengine hatutaki drama za kitoto msi force mambo..” – NandyΒ 

Baada ya kupost hivyo Nandy aliifuta post hiyo kwenye Instagram yake.

UCHEBE KAFUNGUKA KUHUSU SHILOLE KULEWA “Nimembadilisha Shilole hakuwa hivi”

Soma na hizi

Tupia Comments